Adili na Nduguze

by Shaaban Bin Robert


Adili alipofika nyumba nyingine, kubwa kuliko ya kwanza, alifungua mlango akaingia ndani. Nyuma yake mlango utifungwa kwa nguvu. Ikibali alinyata mpaka mlangoni akasimama kimya. Alichungulia ndani katika ufa wa mlango akaona ukumbi. Katika ukumbi palikuwa na kitanda kizuri na meza moja. Manyani yaliyofungwa viunoni minyororo ya dhahabu yalikuwa yamelala kitandani. Adili aliweka sinia juu ya meza. Nyani moja lilipofunguliwa lilirukaruka likalialia kinyonge. Adili alilikamata akalifunga miguu ye mbele na ya nyuma kwa kamba. Alipolitupa chini... Mikasa katika hadithi hii inahusu wanadamu na imesimuliwa kinaganaga. inatazamiwa kuwa kitabu chenyewe kitawapendeza wasomaji wake.

 

ISBN: 9789966344083 SKU: 2010143000605
KES 632
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect