Alama Taanisi ya Kiswahili KCPE

by Abubakar


Alama Taanisi ya Kiswahili: Maswali ya Mazoezi - K.C.P.E ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi mkubwa kwa kusudi la kumwandaa na kumnoa mwanafunzi anayejitayarisha kwa mtihani wa somo la Kiswahili — K.C.P.E. Kitabu hiki kimeandikwa kwa kuzingatia silabasi mpya ya shule za msingi. Pia, kimezingatia msamiati mwafaka na sahihi, miundo, mitindo na mbinu zinazotumiwa katika kuandaa na kutahini Kiswahili, ngazi ya K.C.P.E.

Mwongozo wa uandishi na utahini wa insha pia haujasazwa. Mbinu, mtindo na jinsi ya kuandika insha pamoja na yanayotahiniwa katika insha yameelezwa.

Kwa mwalimu, kitabu hiki ni nyenzo ya kipekee ya kuwatathmini wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa K.C.P.E. Aidha, mwanafunzi atapata rasilimali ya kufanyia mazoezi katika kujiweka tayari kuukabili mtihani. Maandalizi haya ndiyo chanzo cha kupata ‘Alama Taanisi’ katika mtihani.

ISBN: 9789966313096 SKU: 2010127000600
KES 720

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect