Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine

by Iribemwangi


Alidhani Kapata na hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazoshughulikia maswala mbalimbali yanayoziathiri jamii zeta, hususan maswala ibuka kama vile: ufisadi, ukimwi, uhifadhi wa mazingira, unyumba na kadhalika. Aidha, hadithi hizi zimeandikwa na waandishi wenye tajriba tofauti za kimaisha - kuna wale ambao wana tajriba kubwa ki-umri na ki-uandishi, na pia kuna vijana ambao wanaandika kwa mara yao ya kwanza. Pamoja na hayo, diwani hii imejumuisha waandishi wa kiume na wa kike, iimuradi kuzipa jinsia zote nafasi ya kujieieza na kusikika. Ni hadithi ambazo zitasisimua na kuchochea hisia za masikitiko; zitasuta udhaifu wa kibinadamu na pia kutoa mwelekeo ufaao.   

ISBN: 2010127000354 SKU: 2010127000354
KES 653
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect