Almasi za Bandia
Almasi za Bandia ni hadithi ya kisiasa na ya kusisimua inayosimulia juu ya kijana Merton 'aliyehitimu' katika fani hasi ya unafiki na uzandiki. Hata hivyo vijana Yakini na Zambe wanapoingia katika ulingo na kuufichua uovu huu, tishio linaingia - ah, na 'moto' unawaka....
Almasi Za Bandia ni hadithi ya kipekee inayomwezesha msomaji kuuona ulimwengu wa Afrika na Ulaya katika uhalisi wake. Hakika, hatimaye msomaji atabaini kwamba ubandia unaosimuliwa humu si wa almasi tu, bali unawahusu zaidi hao 'wakubwa' waheshimiwao. Hii ni hadithi ambayo mara uanzapo kuisoma, hutapenda kuiacha hadi uimalize!
KES 408

International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect