Dira ya Uandishi wa Insha Mazoezi na marudio kwa Shule za Upili

by KLB


Kuandika ni stadi muhimu katika maisha ya binadamu. Hii ni njia mojawapo anayotumia binadamu kuwasiliana na wenzake kwa insha. Ni kwa kutambua umuhimu huu, ndipo kitabu hiki Dira ya Uandishi wa Insha kinashughulikia kwa ufarisi masuala muhimu yanayohusiana na uandishi kama njia ya kuwasiliana.

Dira ya Uandishi wa Insha ni kurunzi inayomwongoza msomaji kupata njia na mwelekeo ufaao katika uandishi. Kitabu hiki kinashughulikia uandishi wa insha, utungaji wa kiuamilifu, utunzi wa kisanii na uandishi wa tahakiki. Aina zote za insha, sifa zake, mifano tele na mazoezi kemkemu yametolewa. Isitoshe, ili kumwandaa mtahiniwa kwa mtihani wa Kiswahili wa KCSE, mitihani vielelezo ya insha imetolewa.

Kitabu hiki, Dira ya Uandishi wa Insha, ni dira aali kwa wanafunzi na walimu wa Kiswahili wa shule za upili. Aidha, kitawafaa wanafunzi na walimu wa Kiswahili katika vyuo vya ualimu, vyuo vikuu na yeyote anayehusika na utunzi wa hadithi fupi, riwaya, mashairi na tamthilia.

ISBN: 9789966447715 SKU: 2010127000398
KES 580
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect