Get it Right Kiswahili Kidato 1 na 2 marudio

by Kamithi


GET IT RIGHT KISWAHILI KIDATO CHA 1 NA 2 ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi wa kupigiwa mfano. Maarubu ya kitabu hiki ni kuwajengea wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili, msingi thabiti wa kukabiliana na mtihani wa kitaifa (K.C.S.£). Aidha, ni kitabu ambacho kitawafaa pakubwa wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne, wanaotaka kujikumbusha stadi zilizofunzwa katika kidato cha kwanza na cha pili. Kimeandikwa kwa mtindo mwepesi na rahisi kusomeka.

Kitabu hiki kina sifa zifuatazo:

  1.  Kimeshughulikia stadi zote zinazostahili kufunzwa katika kidato cha kwanza na cha pili kwa mujibu wa silabasi.
  2. Kina maelezo ya utondoti ambayo yametolewa kwa lugha rahisi inayowawezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili kuelewa fika vipengele vyote vya: ufahamu, muhtasari, matumizi ya lugha, uandishi wa insha na tungo za kiuamilifu, fasihi simulizi, fasihi andishi na ushairi bila usaidizi wa mwalimu.
  3. Kimetoa mifano maridhawa kwa kila stadi pamoja na mazoezi tele baada ya kila mada ndogo na mada kuu. Aidha, majibu ya mazoezi haya yametolewa ili kurahisisha marudio na uelewa wa mwanafunzi.
  4. Kina mitihani kielelezo inayolenga kunoa makali ya mwanafunzi. Majibu ya mitihani hii yamo kitabuni kwenye kurasa za mwisho.
  5. Mwandishi wa kitabu hiki ni mwalimu mwenye tajriba pevu ya kufundisha Kiswahili. Amefundisha katika shule mbalimbali humu nchini na kupata matokeo bora katika mitihani ya kitaifa.
ISBN: 9789966193421 SKU: 2010127000674
KES 770
International delivery
Free delivery on orders over KSh 
Free click & collect