Harusi ya Wendawazimu

by Thomas


Kila mtu ana wendawazimu wake. Lakini marafiki wawili, Garincha na Chris wanapoamua kufunga ndoa na msichana mmoja, tena kwa ushirikiano na harusi ifanyike hadharani... mchana peupe, tena kanisani itaelezwa kama wazimu wa kiwango gani huo! Huyu msichana mbona awapende wanaume wawili na kukubali kufunga nao ndoa siku moja? Haya ni mapenzi au ni kupagawa? Harusi ya Wendawazimu ni hadithi iliyojengwa kikejeli. Mwandishi anatuletea maswala mbalimbali ambayo hutokea kwenye jamii yetu na ambayo kwa hakika, wakati mwingine watu wenye akili timamu huonekana kama mbumbumbu mara kwa mara wanapofanya vitendo vya kiafkani. Taharuki imetanda kote kutoka mwanzo hadi mwisho wa hadithi. Kila anayeanza kukisoma kitabu hiki huchoma hadi tone la mwisho la mafuta katika kibatari kusudi "...ashiriki Harusi ya Wendawazimu hadi tamati."

 

ISBN: 9966361227 SKU: 2010143000691
KES 458
International delivery
Free delivery on orders over KSh 0
Free click & collect

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review