Kamusi Changanuzi ya Methali

by Gichohi Waihiga, francis M.Kagwa


KAMUSI CHANGANUZI YA METHALI  ni kitabu chenye mkusanyiko mkubwa zaidi wa methali kikilinganiishwa na kamusi nyingine mbalimbali zilizowahi kuiayarishwa kufikia sasa. Lakini la muhimu zaidi. licha ya wingi wa methali, kitabu hiki kinayo haiba, mnato na muundo wa kipekee unaokifanya kuvutia jicho la kila msomaji. Isitoshe. methali zilizomo zimechanganuliwa kwa lugha rahisi inayoeleweka na wapenzi wa lugha hii wa viwango vyote.

Kwa jumla kinazo sifa zifuatazo.

  • Mkusanyiko wa zaidi ya methali elfu mbili na mia nne.
  • Methali halisi zisizo za kubambanya zilizopangiliwa kwa utaratibu wa kialfabeti kuanzia A hadi Z.
  • Maelezo kamili ya msamiati mgumu uliomo.
  • Maelezo kamili ya maana ya  kila methali 
  • Maelekezo kamili ya matumizi ya kila methali.
  • Methali zenye maana sawa au  kinyume na  nyingine zimedhihirishwa na kuelekezwa kurasa zipatikanamo.
ISBN: 9789966342638 SKU: 2010127000364
KES 980
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect