Kamusi ya Semi-Toleo Jipya

by Ndalu, Kingei


Toleo Jipya Ia Kamusi ya Semi ndicho kitabu cha pekee kilichokusanya zaidi ya semi elfu nne. Kitabu hiki kinajumuisha semi, maana yake, pamoja na mifano faafu. Ufafanuzi wa msamiati umetiliwa maanani huku maana kadhaa za semi zikitolewa. Aidha, semi zilizomo humu kitabuni zimepangwa kialfabeti ili kurahisisha urejeleaji. Toleo hili Jipya Ia Kamusi ya Semi ni kitabu kinachowafaa wanafunzi na walimu wa kila daraja: shule za msingi, za upili na hata vyuo vikuu. Hii ni dafina kuu kwa wapenzi wote wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Kitula King'ei ni mwalimu, mwandishi, mtafiti na msomi wa lugha na fasihi ya Kiswahili aliye na tajriba kubwa sana. Kwa sasa, ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ahmed Ndalu amefundisha Kiswahili katika shule za upili na vyuoni, na vile vile kuandika vitabu kadhaa. Hivi sasa, amestaafu kazi ya ufundishaji na anajishughulisha na utafiti na uandishi wa vitabu vinavyoshughulikia nyanja tofauti tofauti za Kiswahili. 

ISBN: 9966465405 SKU: 2010127000334
KES 796
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect