KCPE Homestretch Insha Kamili
by Zack Yaona
KCPE Homestretch ni msururu wa vitabu vya marudio vinavyolenga kuimarisha matokeo ya wanafunzi katika mtihani wa KCPE.
Utamu wa Kiswahili ni ufasaha katika kuandika na kutamka. Kitabu ambacho wapenzi wa Kiswahili wamekuwa wakikisubiri kwa hamu na hamumu ndicho hiki, KCPE Homestretch insha Kamili. Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Kiswahili, kimetokea kitabu ambacho:
- Mpangilio wacho hauna kifani. * Kina mifano mingi na kamili.
- Kinatimiza mahitaji ya silabasi. * Ni chepesi na rahisi kuelewa.
- Kina ufasaha wa hali ya juu. * Kinaenda na wakati.
Ukiwa na kitabu hiki hutakosa kufurahia mambo kadha wa kadha kama vile:
- Ubunifu wa kupigiwa mako.
- Mwongozo mpya wa kusahihisha KCPE.
- Maelezo kamili, mepesi na sadakta.
- Kupata alama za juu Zaidi katika insha (40/40).
- Kugundua mwandishi mzuri ni mwalimu mzuri.
Kwa mara nyingine tena Zake Yaona amefanya mambo. Mwandishi huyu wa kisasa asiyependa ukasuku, utumizi wa maneno kivoloya wala uzembe, amedhihirisha ustadi wake katika kuwaza, kubuni na kuandika vitabu anuwai. Amefundisha katika shule kadhaa. Kwa sasa ni mchambuzi mkuu wa silabasi mpya na mshauri katika masuala ya silabasi/mtaala na mtihani wa KCPE.
