KCPE Made Familiar: Kitabu cha Mazoezi Kiswahili 2024 (New Edition)
Kitabu hiki cha mazoezi ya Insha kimeandaliwa mahsusi ili kuwasaidia wanafunzi katika shule za upili kudurusu na kuelewa kwa undani mada inayofunzwa darasani kwa kujibu maswali yaliyo katika kitabu hiki kutoka katika hiyo mada. Kwa njia hii, kitabu kitawasaidia wanafunzi kutambua kile wanachofunzwa darasani na K.C.P.E.Kitabu hiki pia ni chenye manufaa makubwa kwa walimu ambao wangependa kuwaonyesha wanafunzi wao jinsi maswali huulizwa katika mtihani kwa kuzingatia mada mbalimbali. Kitabu hiki kina maswali kuhusu mada zinazofunzwa katika darasa cha 4, 5, 6, 7 na 8. Pia kuna dhana - mseto ambazo zinafunzwa katika darasa chochote. Majibu yaliyo baada ya maswali yanakusudiwa kumnoa na kumsukuma mwanafunzi kufaulu kwa kujisomesha mwenyewe (kuwa mwalimu wake binafsi).