Kidagaa Kimemwozea


 Toleo la Shule "Kila kazi kuu ya fasihi huwa imejengwa katika misingi ya sitiari ya safari; na katika riwaya hii ya mawanda ya kiepiki, Ken Walibora katupatia mojawapo ya kazi hizo kuu za fasihi. Kidagaa Kimemwozea imejaa ucheshi sambamba na majonzi. Ni riwaya iliyojaa mijadala mizitomizito ya masuala ya kijamii, iliyojificha katika ucheshi, sitiari, taswira, na tashtiti. Kwa kupitia mbinu kadhaa za kisanaa, ikiwemo ya vitabiri na mara mojamoja virejeshi, Ken Walibora kaonyesha tena ufundi wake mkubwa wa kutuchorea hali halisi za wanyonge wanyongwao. Ha, hawa ni wanyonge ambao hatimaye wanaamua liwalo na liwe. Kidagaa Kimemwozea ni riwaya ambayo anwani yake inatuachia maswali mengi: Nani huyo ambaye kidagaa kimwemwozea? Jina la riwaya hii linatufanya tujiulize je, huyo ambaye kidagaa kimemwozea, kimemwozea vipi wakati si rahisi kwa dagaa kuoza? Kwa namna gani,na kwa nini? Hi kuyajibu maswali haya, inatubidi tuungane na wahusika wake kwenye safari ya kujisaka,turudi nyuma na kuanza kuisoma tena upya riwaya hii ambayo ukianza kuisoma huwezi kuiweka chini. "Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ni miongoni mwa riwaya bora zaidi za Kiswahili zilizowahi kuandikwa. Kwa mara nyingine tena katika lugha tamu na kwasi Ken Walibora ameoanisha fani na maudhui kwa umahiri wa aina yake. Almuradi riwaya hii imesukwa ikasukika, ikapikwa ikapikika na kuandikwa ikaandikika."   

Out of stock
KES 100

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect
SKU2010129000134

Reviews

Average rating: 5

from 1 review

5 1 five star review
4 0 four star reviews
3 0 three star reviews
2 0 two star reviews
1 0 one star reviews
Add your review

edwin reviewed on 1 Feb 2020

2 of 2 customers found this useful.

kidaga kimemuozea

great story not only entertaining but also with great moral value and clear reflection of our society today great work ken walibora

Add your review