Kivukio cha Uandishi Bora wa Insha

by Maina


KIVUKIO CHA UANDISHI BORA WA INSHA ni kitabu ambacho kimeandaliwa na kuandikwa baada ya utafiti wa kina. Kimeazimia kuwaauni wanafunzi na wapenzi wote wa lugha kuvuka na kufikia upeo wa kuzungumza Kiswahili sanifu na k-uandika insha aaliaali. Sarufi imesarifiwa na msamiati mwafaka kuimarishwa. Mtindo wake ni wa kipekee unaojumuisha vipengele muhimu mathalani: Uandishi wa insha, Uakifishaji, Aina za maneno, Ngeli za majina, Tamathali za lugha, Tamathali za uandishi, Matumizi ya visawe, vitawe na vitate, Usahihishaji wa insha na Aina za insha.  Insha zilizo katika nakala hii zimeandikwa kwa ubunifu na ustadi wa hall ya juu sang. Mwongozo wa kila sehemu muhimu zinazozingatiwa katika insha umeelezewa ipasavyo. Mwandishi wa kitabu hiki amebobea na kutaratamba kwa tajriba pevu na pana katika ufunzaji wa lugha ya Kiswahili. Kwa majaaliwa ya Mola amefanikiwa kuwafaa watahiniwa wa ngazi tofauti na kuwasaidia kufua dafu katika mitihani yao. Ni mmojawapo wa waalimu adimu wanaoshikilia rekodi ya kuwa na matokeo bora zaidi nchini.   

ISBN: 9789966156822 SKU: 2010127000508
Out of stock
KES 370

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect