KLB Skillgrow Mazoezi ya Lugha Hatua ya 2


KLB Skillgrow Mazoezi ya Lugha Hatua ya Pili (Kaaba cha Mwanafunzi) ni kitabu mojawapo kati ya vitabu vinavyochapishwa na Kenya Literature Bureau vya msururu wa Skillgrow. Msururu huu wa vitabu umezingatia Mtalaa wa kiumilisi wa mwaka wa 2017 wa masomo ya shule za Nasari. 

Kitabu hiki kimekusudiwa kumwezesha mwanafunzi kukuza uwezo wa kutumia stadi zote nne za lugha ya Kiswahili; Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na kujiandaa Kuandika. Kupitia stadi hizi, mwanafunzi anakuza uwezo wake wa lugha. 

Toleo hili limejumuisha mambo muhimu ambayo yanachangia ujifunzaji wa sasa ambayo ni masuala mtambuko, maswali dadisi, masuala ya jinsia, picha murua za kuchangamsha na kuibua hamu ya kudadisi kwa mwanafunzi na mbinu tofauti za kumwezesha mwanafunzi kukuza uwezo wake wa kujifunza. Mazingira halisi ya mwanafunzi yamezingatiwa katika kukuza kazi hii. Hili linamwezesha mwanafunzi kujifunza katika hali halisi. Lugha sahili imetumika ili kurahisisha kuelewa kwa mada zote katika kitabu hiki. 

KES 278
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect
UPC2010127000732
Author KLB
ISBN 9789966652010
Weight (kg) 0.3
SKU2010127000732

Reviews

Leave a product review
or cancel