Longhorn Kiswahili Mufti GD 2

by Wallah


Longhorn Kiswahili Mufti, Gredi 2 (Kitabu cha Mwanafunzi) ni kitabu kilichoandikwa kwa mtindo wa mazoezi kwa kuzingatia mtaala mpya unaokusudiwa kujenga ujuzi wa mwanafunzi kupitia utendaji na uvumbuzi wa maarifa. Kitabu hiki kimetimiza kikamilifu mahitaji ya mada zote za silabasi mpya ya somo la Kiswahili kwa wanafunzi wa gredi ya pili.

Vilevile, kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha rahisi ili kueleweka kwa urahisi na. wanafunzi wa gredi ya pili kutoka katika mazingira mbalimbali. Msamiati uliotumika unaafikiana vyema na uwezo wa lugha ya wanafunzi katika kiwango hiki. Kimeshughulikia masuala ibuka kama vile: usalama, maadili, lishe bora, usafiri, utangamano, maarifa ya ujasiriamali, elimu endelevu, jinsia, teknolojia na mazingira. Pia, michoro ya kuvutia imetumiwa ili kumsaidia mwanafunzi kufahamu yaliyomo kwa urahisi na kuweza kuyahusisha maarifa na mazingira yake.

Kitabu hiki kina mwongozo wa mwalimu ambao utampa mwalimu maelezo na maelekezo kamili kuhusiana na mbinu mwafaka za kutayarisha, kuendesha na kutathmini uwezo wa utendaji wa wanafunzi na umahiri wao katika somo la Kiswahili.

ISBN: 9789966640031 SKU: 2010127000741
KES 540
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect