Longhorn Kiswahili Mufti GD3 Mwalimu

by Wallah


Longhorn Kiswahili Mufti, Gredi 3 (Mwongozo wa Mwalimu) ni kitabu ambacho kinampa mwalimu maelezo na maelekezo kamili kuhusiana na mbinu mwafaka za kutayarisha, kuendesha na kutathmini uwezo wa utendaji wa wanafunzi na umahiri wao katika somo la Kiswahili. 

Mwongozo huu umeandikwa kwa kuzingatia mtaala mpya unaokusudiwa kujenga ujuzi wa mwanafunzi kupitia utendaji na uvumbuzi wa maarifa. Pia, mwongozo huu umetimiza kikamilifu mahitaji ya mada zote za silabasi mpya ya somo la Kiswahili kwa wanafunzi wa gredi ya tatu. 

Vilevile, mwongozo huu una mifano mwafaka ya maazimio ya kazi, mpangilio wa funzo na ratiba ya vipindi itakayomwongoza mwalimu kuzingatia mbinu zinazofaa za kutekeleza malengo yote ya somo la Kiswahili kwa gredi ya tatu. Pia, mwongozo huu una majibu ya mazoezi na maswali ya marudio yote yaliyomo katika kitabu cha mwanafunzi. 

ISBN: 9789966640079 SKU: 2010127000782
Out of stock
KES 485

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect