Longhorn Mwanga wa Kiswahili GD4 Mwalimu (Appr)


Longhorn Mwanga wa Kiswahili Gredi ya 4 (Mwongozo wa Mwalimu) ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi na umahiri mkubwa kwa 
ajili ya mwalimu na mlezi wa mwanafunzi wa gredi ya nne. Kinatosheleza kikamilifu mahitaji ya mtaala mpya wa umilisi 
pamoja na malengo ya elimu ya taifa la Kenya. Kitabu hiki ni silaha tosha kwa mwalimu kwa jinsi kinavyomwelekeza kujitayarisha, kufundisha na 
kutathmini umilisi mbalimbali wa mwanafunzi katika somo la Kiswahili.
Mwalimu ameelekezwa kikamilifu jinsi ya kufundisha na kutathmini shughuli zote zilizopendekezwa katika kitabu cha 
mwanafunzi. Namna ya kuwashughulikia wanafunzi walio na mahitaji maalum pamoja na wanaoishi katika mazingira mbalimbali 
pia imeangaziwa katika kila mada kuu.
Majibu tarajiwa kwa shughuli zote, kazi za ziada pamoja na mazoezi yaliyomo katika kitabu cha mwanafunzi yametolewa katika kila mada.
Pia, kitabu hiki kina vielelezo mwafaka vya maazimio ya kazi, mpangilio wa somo, rekodi ya ufunzaji, rekodi ya maendeleo 
ya wanafunzi pamoja na maelezo ya kina kuhusiana na utekelezaji wa mtaala mpya wa umilisi.
Isitioshe, waandishi wa kitabu hiki ni walimu na watahini wenye ujuzi wa kutosha katika ufundishaji na utahini wa Kiswahili kwa miaka mingi.

ISBN: 9789966642912 SKU: 2010127000824
KES 500
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect