Longhorn: Shada na Mwili Wake Grade 1

by Mwebi


Shada, Sudi na marafiki zao wanapenda kucheza pamoja kila Jumamosi. Jumamosi hii, mama anawaita Shada na wenzake kula chakula cha mchana. Baada ya kula na kurudi kucheza, Shada anashikilia tumbo lake na kuanza kulia kwa sauti. Je, ni yepi yamempata Shada? Wenzake wanamsaidiaje?

Hadithi Mufti za Longhorn ni mfululizo mpya wa hadithi ambazo zimeandikwa kulingana na mtaala mpya. Hizi hadithi zinalenga kukuza ujuzi wa wanafunzi kupitia kwa uvumbuzi wa maarifa na zinaimarisha uelewa wao wa masuala ibuka katika jamii. Hadithi hizi sio tu za kuelimisha na kuburudisha, bali pia zimeambatanishwa na mazoezi ambayo yatawasaidia wanafunzi kuimarika kiubunifu, kimawazo na kifikra.

ISBN: 9789966641953 SKU: 2010143001089
KES 230