Majaribio ya Mtihani KCPE Kiswahili
by J. Mwashigadi, T, Abubakar, H. Mwangi, J. Ndege, J. Maloba
Kitabu hiki chenye sampuli hamsini za mtihani wa KCPE kwa mujibu wa silabasi mpya, kinalenga kumwandaa na kumnoa mwanafunzi barabara kwa mtihani. Kila karatasi kwenye kitabu hiki imeandaliwa kitaalam kwa kuzingatia msamiati, miundo, mitindo na mbinu zinazotumiwa katika kuandaa mitihani ya KCPE, ili kumweka tayari mwanafunzi kukabiliana na utelezi na changamoto katika maeneo yote ya KCPE—Kiswahili.
Kwa mwalimu, kitabu hiki ni nyenzo ya kipekee ya kuwatathmini, kuwaboresha na kuwaandaa wanafunzi kwa mtihani.
Bila shaka, mwanafunzi anayejiandaa kwa kutumia kitabu hiki, afikiapo mtihani wenyewe, hali yake haina tofauti na ile ya mwogeleaji wa maji makuu baharini kupewa 'changamoto' ya kubainisha umahiri wake kwenye kidimbwi.
