Marudio ya Nyota ya Kiswahili KCPE Maswali na Majibu

by Eliud Murono, Joseph Mwamburi


Marudio Nyota ya Kiswahili KCPE ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi mkuu kwa kusudi la 
kumwandaa na kumnoa mwanafunzi anayejitayarisha kwa mtihani wa somo la Kiswahili - KCPE. 
Kitabu hiki kimeandikwa kwa kuzingatia silabasi mpya ya shule za msingi. 
Kimezingatia msamiati mwafaka na sahihi, miundo, mitindo na mbinu zinazotumiwa katika 
kuandaa na kutahini Kiswahili katika ngazi ya KCPE.
Vipengele muhimu vilivyoshughulikiwa katika kitabu hiki ni: 
• Kusikiliza na kuongea: Maamkizi na adabu, mashairi n.k.
Sarufi: Ngeli, aina mbalimbali za maneno, virejeshi, viambishi n.k. Matumizi ya Lugha: 
Vitendawili, methali, tashbihi, tanakali za sauti n.k.
Msamiati: Wizara mbalimbali, sayari, vikembe, pembe za dunia, malipo n.k. 
• Kuandika: Aina za barua, insha za methali, maelezo, masimulizi, dondoo n.k.
Mazoezi: Mazoezi kwa kila kijimada kilichotolewa maelezo. 
Karatasi sampuli za KCPE: Karatasi zipatazo ishirini zenye muundo wa KCPE. 
Majibu: Majibu ya mazoezi yote pamoja na ya karatasi za sampuli za KCPE.
Aidha, mwanafunzi atapata rasilimali ya kufanyia mazoezi katika kujiweka tayari kuukabili 
mtihani bila woga wowote. Maandalizi haya ndiyo chanzo cha kuwa 'Nyota' katika mtihani wa KCPE.
Kwa mwalimu, kitabu hiki chenye mazoezi mengi, karatasi sampuli za KCPE pamoja na majibu yake ni 
nyenzo ya kipekee ya kuwatathmini, kuwaboresha na kuwaandaa wanafunzi kwa mtihani wa kitaifa.
 

ISBN: 9789966313904 SKU: 2010127000662
Out of stock
KES 720

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect