Mashetani Wamerudi

by Said A Mohamed


Profesa-Haft-Leo-Wala-Kesho ni mwenye kipaji cha kusema na kuwavuta watu - hasa vijana. Mhusika huyu anatumia kipaji chake kutetea na kupinga 'mkwamo' katika Dunia ya Tatu - ikiwemo Afrika. 'Mkwamo' huo, ulianza mwanzoni mwa ukolonikale na kushamiri katika ukolonimamboleo. Kwa ajili ya 'mkwamo' huo, Afrika imetupwa na kuachwa nyuma kwa kila kitu, hasa katika kunyonywa jana, leo na kesho.

Mashetani Wamerudi ni tamthilia inayoleta mivutano pande mbili: upande wa mashetani na vibaraka vyao, na upande wa vijana na wazee wanaochachamaa. Mwisho wa mvutano, Profesa Hafi-Leo-Wala-Kesho anakufa kifo cha ajabu na kuleta tanzia pamoja na tamaa ya kuamsha silaha ya ukombozi! Tamthilia hii ina mchovyo unaosimamia maana mbili: maana ya kijujujuu yenye lugha ya kificho, na maana ya pill yenye kuleta lugha ya ukinzani na vijembe ndani ya lugha ya mtindo wa usasa, inayoipa hadhira mitazamo mbalimbali kwa wasomaji. Katika mtindo huu, kung vuta nikuvute, mtindo unaoburudisha na kuhuzunisha, inayorambwa ndani ya 'asali chungu' na utamu wa mchezo wa sitiari, ishara, mafumbo, usambamba, kejeli na mgao unaofuata mapigo ya ushairi na uwazi wa nathari. Said A. Mohamed ni mwandishi wa fasihi mwenye ukwasi mpevu na tajriba kubwa. Kazi zake zinajumuisha diwani za mashairi,diwani za hadithi fupi,riwaya na tamthlia.

ISBN: 9789966570321 SKU: 2010129000184
KES 487

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect