Mazoezi na Marudio Mufti ya Kiswahili 7

by Wallah Bin


Mazoezi na Marudio Mufti ya Kiswahili, Darasa la 7 ni kitabu kilichoandikwa kwa weledi mkuu kwa madhumuni ya kumwandaa na kumnoa mwanafunzi anayejitayarisha kwa mtihani wa somo la Kiswahili - K.C.P.E. Kitabu hiki kimeandikwa kwa kuzingatia silabasi mpya ya shuleza msingi. Kinalenga kuhamasisha na kupiga msasa usasa wa kutoa mazoezi na marudio kwa wanafunzi na wote wanaosoma lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki, ujirani wake na kote ulimwenguni.Kitabu hiki kimezingatia msamiati mwafaka na sahihi, miundo, mitindo na mbinu zinazotumiwa katika kuandaa na kutahini somo la Kiswahili katika ngazi ya K.C.P.E.Kwa mwalimu, kitabu hiki chenye karatasi themanini (80) za maswali ya mazoezi ya K.C.P.E pamoja na majibu yake ni nyenzo ya kipekee ya kuwatathmini, kuwaboresha na kuwaandaa wanafunzi kwa mtihani wa kitaifa. Katika maswali haya mna mazoezi ya mazoea, uzoefu na kuzoesha ili mwanafunzi au yeyote akitumiaye kitabu hiki apate kichocheo, mwamko na hamu kiasi cha kwamba akimaliza zoezi moja aendelee kufanya jingine na jingine hadi ajikute amekuwa mzoefu wa mazoea ya kufanya mazoezi ya Kiswahili Mufti.Vivuto na vivutio halisi katika kitabu hiki ni jinsi maswali yalivyoulizwa kwa namna ya kuchangamsha na kudadisisha. Fauka ya hayo, vifungu vya ufahamu vina upekee kwa maana ya kuhekimisha, kushajiisha, kunasihi na kuarifisha, kwa maarifa kemkemu.

ISBN: 9789966318398 SKU: 2010127000621
KES 825

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect