Mbaya Wetu

by Ken Walibora


Mbaya Wetu ni tamthilia ya kijamii inayoangazia kitashtiti suala la malezi. Tamthilia hii inamulikia kurunzi taasisi ya familia, vyombo vya dola na jamii kwa jumla na kufichua utepetevu katika utekelezaji wa majukumu ya kimsingi. Matokeo ya utepetevu huu na kuthamini wasiothaminika ni kuibuka kwa wanajamii ambao hawawezi kuihakikishia jamii yao mustakabali ufaao. 

Tamthilia hii yenye ucheshi na ubunifu wa aina yake inahusu hatima ya Matari na jamii yake. Matari ni kitindamimba aliyedekezwa na wazazi wake na jamii kwa jumla. Kudekezwa huku kuna athari gani kwa mdekezwa na wadekezaji? Je, Matari anajihasiri na kuwahasiri wengine kwa kiasi gani? Nao wanajamii watakubali hasara mpaka lini? 

ISBN: 9789966347794 SKU: 2010129000160
KES 330
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect