Mkasa wa Shujaa Liyongo

by Bitungi Matundura


MKASA wa SHUJAA LIYONGO ni hadithi inayomulika kinyang'anyiro cha uongozi kati ya ndugu wawili: Liyongo na Daudi Mringwari. Baba yao Fumo anapofariki kutokana na ugonjwa, wanaanza kung'ang'ania uongozi wa Jimbo la Shanga. Mvutano huu unaishia katika kifo cha Liyongo mikononi mwa mtoto wake Moni. Liyongo Fumo aliishi karne nyingi zilizopita katika pwani ya Kenya na alikuwa mshairi maarufu. Mvutano unaosimuliwa katika hadithi hii ulitokea, ingawa pengine kwa njia tofauti kidogo. Katika kuuhadithia, mwandishi ameupa mwamko mpya wa kisanaa. Mwandishi wa hadithi hii, Bitugi Matundura, alifuzu somo la Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Moi mwaka 1999. Ameandika hadithi nyingi za watoto, hasa katika gazeti la Taifa Leo.   

 

ISBN: 9966472274 SKU: 2010143000151
KES 289
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect