Moran Stadi za Kiswahili Shugli za Lugha Kitabu cha Mwalimu Gredi 2 (Approved)

by Moran


Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwalimu, Gredi ya 2 ni mwongozo unaomwelekeza mwalimu kuendesha vipindi vya Kiswahili darasani. Kwa mintarafu ya mtaala mpya uegemedo umilisi uliozinduliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD) mnamo Septemba 2017 na uliotumiwa kukiandaa kitabu hiki, mwalimu ni mwezeshaji wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Mwongozo huu umetayarishwa kwa kutilia maanani ukweli huu.

Mwalimu amependekezewa jinsi ya kuandaa masomo, mbinu, zana na vifaa, utaratibu wa ufundishaji na jinsi ya kupima kiwango cha umilisi wa mwanafunzi baada ya kila kipindi. Aidha, Mwalimu amependekezewa jinsi ya kusimamia shughuli za mwanafunzi binafsi, za wanafunzi wawiliwawili na hata za makundi ya wanafunzi. Aidha, majibu ya mazoezi yaliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi yametolewa katika mwongozo huu.

Katika kila kipindi, mwalimu amependekezewa jinsi ya kuhusisha ‘stadi nne kuu Za lugha: kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Si hayo tu, ameelekezwa jinsi ya kuoanisha mada mbalimbati na umilisi wa kimsingi, masuala mtambuko, maadili, uhusiano wa mada mbalimbali na masomo mengine miongoni mwa masuala mengine yanayofumbatwa na mtaala mpya uegemedo umilisi.

Azma ya mwongozo huu ni kumchochea mwalimu kuwa mbunifu katika kuendeleza vipindi vya Kiswahili. Hivyo, ataweza kumtayarisha mwanafunzi wa Gredi ya 2 kutumia Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali kwa kujithamini na kujiamini.

ISBN: 9789966630315 SKU: 2010127000699
Out of stock
KES 340

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect