Msururu wa Fataki: Nargisi michongomani

by Nzaro


Sadakta! Nakubali kuwa ni sharti kila mpigambizi aamini kwamba bahari haishi zinge. Kama hayo ya wanamaji utayakwepa na kuhamia nchi kavu, huko pia ni duniani; nayo dunia huleta vyema na vimbi. Hayo ndiyo anayokabiliana nayo kila mtu mwenye azma. Mvita aliyaona, akayaonja na kukiri, “Hakika nitafaulu. Acha hii michongoma iliyonizingira iniondokee, uone jinsi nargisi yangu itakavyonawiri na kutema marashi yake kila mahali” 

Nargisi Michongomani ni riwaya inayotekenya hisia za kila msomaji. Yaani, ni mchanganyiko maalumu utakaokupiga bumbuazi katika mnuno hadi kilio na kutanabahia katika tabasamu hadi kicheko. Vyote hivyo vilisukwa kwenye ukili mmoja kwa ufundi wa kipekee utakaompa burudani safi kila msomaji.

Johnson Nzaro amehitimu mafunzo katika somo la Kiswahili na kukabidhiwa shahada katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Hivi sasa, Nzaro ni mtaalamu mwenye tajiriba pana katika uandishi na ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Kenya.

ISBN: 9789966068293 SKU: 2010143000953
KES 499
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect