Mwisho wa kosa


Sura 1 Monika anarejea kutoka ulaya alikokwenda kusoma. Waliokwenda kumlaki wanaonyeshwa dharau pale uwanja wa ndege.Tunaelezwa kuhusu kesi ya Asha na Bi keti amabapo katika Uk 29 Keti anakamatwa na polisi na kesi yao kuanza. Monika wanazozana na keti kuhusu uji. Sura 2 Tunaelezwa mpango wa wazazi wa Ali juu ya ndoa ya Ali na Zabara uk 54.Tunaelezwa jinsi ndugu na dadake zake Ali wanavyosumbuliwa na wasichana pale kijijini. Sura ya 3 Monika na Muna wanakutana.Hawa ni wasichana wawili ambao wamesoma.Uk 55 kuna mazungumzo kati ya monika na Muna ambapo Monika anamuuliza Muna maswali juu ya ndoa yake. Ugomvi baina ya Monika na Babake. Na Monika anaondoka kwao.Pia kuna ugomvi kati ya Rashid na Monika wanapoishi pamoja. Sura ya 4 Katika hii sura maudhui ya ufisadi yanajitokeza. Ufisadi kati ya Rashid na Alison.Ambapo Alison anapata kandarasi .Pia Mheshimiwa anataka kumhonga Rashid ili apate kandarasi pia.Tunaelezwa Kazi ya Rashid katika ofisi yake. Sura ya 5 Monika anakutana na Mheshimiwa Selemani na kuuelewa unafiki wa Juma. Tunaelezwa jinsi masomo ya Ali na jinsi madawaya kulevya yalimfanya afukuzwe shule.Uk 121 kuna barua ya kufukuzwa kwa Ali kutoka chuo kikuu. Sura ya 6 Rashid anaenda kwa Saidi kupata ushauri,anahisi kuwa alikosea kwa kushiriki ufisadi.Mhaji anamtemebelea Selele na kumuomba amzungumzie Monika na amsaidie Monika kama mwanawe.Mhaji anataka monika aunganishwe na familia yake. Sura ya 7 Karne anamsaidia Ali katika kazi yake mpya. Karne anaeleza kosa la shilingi 17,000 badala ya shilingi 1700.Hii ni hadithi ndani ya riwaya. Kuna maelezo juu ya ugomvi wa Muna na Hasani katika ndoa yao mabayo in matatizo mengi mno. Sura ya 8 Ali anapata kazi mpya ofisini kwa Alison. Waziri Salimu anashindikizwa kumfuta kazi Rashid.Baadaye Rashid anapata kazi katika kampuni ya Alison. Uk 199 Monika anahama kwa Rashid na kwenda kwa nyumba mypa aliyopewa ma Matata. Kuna ugomvi kati ya Matata na selemani kuhusu Monika. Sura ya 9 Ndoa ya Hasani na Muna ambayo imejaa ugomvi inavunjika na Muna kurudi kwao. Sura ya 10 Matata namuacha Monika na Kuoa msichana mwingine.Monika anarejea kwao na kuolewa na Shabani.Ali na Sara wanapata kujuana na Kupanga kuoana. Riwaya inakamilka kwa sherehe nyumbani kwa Selele.Rashid anakuja na Salama,Monika na Shabani, Muna na Hasani.
KES 696
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect
SKU2010143000164

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review