Mwito wa moto

by Story Moja

by Maina


Tieni na ndugu zake wamekaa chumbani mwa nyanya yao wakingoja chakula chao kiive. 
Akiwa huko jikoni, Tieni anasikia sauti zikimwita kutoka kwenye moto. 
Mababu wanamwita kwenye moto! Wanamvuta karibu zaidi na zaidi! Je, ataanguka kwenye moto?
Vitabu vya Storyhippo ni vya kisasa vilivyojaa vichekesho. 
Vimetungwa katika mazingira ya Afrika Mashariki kwa kuwatia watoto hamu ya kusoma vitabu vingi.
Katika jitihada za kukuza desturi ya usomaji, wazazi wanahimizwa kuwaelekeza watoto wao kwa njia zifuatazo:
1. Kumnunulia mtoto kitabu cha kusoma kulingana na kiwango
chake. Kitabu kikiwa rahisi sana kwa mtoto kusoma, hamu yake ya kusoma itashuka. Vilevile, 
kitabu kikiwa kigumu kupita kiasi mtoto atachoka kukisoma.
2.
Kumshawishi mtoto awe na hamu ya kujua anachokisoma. Mhimize akueleze ama ajadili kile alichokisoma.
3. Kumpongeza mtoto mara kwa mara anaposoma kitabu.
4. Kumnunulia mtoto vitabu vya aina tofauti tofauti ili kuongeza
ufahamu wake na kuongeza hali yake ya kupenda kusoma.
5. Kuzua hamu ya mtoto ya usomaji kwa kuvisoma vitabu vyako
mwenyewe ukiwa nyumbani. Kitendo hiki kitaongeza hamu ya mtoto kusoma na kupata maarifa zaidi. 
Mtoto akijihami na vitabu vya kumfundisha, apate pongezi na uelekezi kutoka kwa wazazi, 
atakuwa mweledi na mpenzi wa usomi.

ISBN: 9789966066961 SKU: 2010143000824
KES 420
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect