Mzalendo Kimathi


Mengi yameandikwa juu ya kiini cha mapambano baina ya Mau Mau na vikosi vya wakoloni Waingereza. Je, kiini hiki kimezungumziwa vya kutosha katika fasihi ya Kenya? Kwa nini fasihi hii imewadunisha wazalendo na kuwafanya wasioweza kuiunda historia yao? Kwa nini waimbaji wetu Kenya hawajapata kuimba nyimbo za kuwasifu mashujaa kama Dedan Kimathi na ujasiri wao? Historia na matendo waliyoyaandika wanahistoria na waandishi wengine ni ya nani? 

Haya ni baadhi to ya maswali yaliyowafanya Ngugi wa Thiong'o na Micere Githae Mugo kuandika mchezo wa Mzalendo Kimathi, mchezo wa aina ya pekee unaoonyesha mapambano ya Kenya katika harakati za kujikomboa. Mhusika mkuu ni Kimathi, kiongozi shupavu wa mapinduzi ya Mau Mau. ingawa anateswa kwa aina nyingi, Kimathi anagoma kabisa kujisalitisha na Ubeberu wa Waingereza. 

KES 300
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect
UPC2010143000737
Author Ngugi wa Thiongo
ISBN 9789966461056
Weight (kg) 0.3
SKU2010143000737

Reviews

Leave a product review
or cancel