Nyota Njema Mawinguni

by Spotlight Publishers


Nyota, ambaye ni mhusika mkuu, anazaliwa na kukua katika mazingira ya kutatanisha. Rangi ya ngozi yake ambayo ni tofauti sana na ya wazazi wake inabadilisha mkondo wa maisha yake. Mkondo huo wa maisha unasawiriwa na mwandishi kwa uketo na uhondo wa lugha yenye ubunifu iii kufichua na kupiga vita maovu ya kijamii na kisiasa. Maovu hayo ambayo yamekita mizizi katika jamii ni kama ubaguzi, ugaidi, ufisadi katika ugatuzi, wizi wa mitihani na utepetevu katika uchaguzi wa haki na kidemokrasia. Uozo huu unarandana na yale madhila yanayoathiri mataifa mengi ulimwenguni. 

ISBN: 9789966570291 SKU: 2010129000186
KES 522
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect