One Planet KPSEA Mwenge wa Kiswahili Gredi 4-6

by One Planet


KPSEA Mwenge wa Kiswahili: Kitabu cha Marudio kimeandikwa kutoa mwongozo na kutatua changamoto za ujifunzaji na tathmini katika Mtaala wa Umilisi. Kitabu hiki kimeshughulikia mada, stadi za lugha na matokeo maalum yanayotarajiwa kwa mtindo rahisi unaomwezesha mwanafunzi kuzimudu shughuli za ujifunzaji hata akizikabili peke yake.

Upekee wa kitabu hiki uko katika uwezo wacho wa kukabili mada na mada ndogo kwa kumpa mwanafunzi na mwalimu shughuli au mazoezi yanayomwezesha kujifunza, na hapo hapo angjitathmini. Kitabu hiki kinamwandaa mwanafunzi, si kwa tathmini endelevu za kila siku katika mchakato wa kawaida wa ujifunzaji, bali pia katika tathmini za hapo shuleni, na muhimu zaidi, katika Tathmini ya Mwisho wa Gredi ya Sita (KPSEA). Tathmini zilizotolewa katika kitabu hiki zinahusisha masuala ambayo mwanafunzi anakumbana nayo kila siku. Zaidi tathmini hizi zinalenga kukuza stadi za karne ya ishirini na moja, na umilisi wa kimsingi, kama vile uwazaji wa kina na utatuzi wa matatizo, mawasiliano, uraia na kujiamini.

ISBN: 9789914410617 SKU: BK00000007742
KES 870
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect