OUP Kiswahili Dadisi Grade 5 Mwalimu (Approved)

by J. Ndege, E. Osoro and Z. Mucheria


Kiswahili Dadisi Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 5
Kiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa njia ya kipekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika, na vilevile sarufi kama ilivyopendekezwa katika mtalaa.
Vitabu katika msururu huu vina mazoezi murua ambayo yatamchangamsha mwanafunzi na kumpa hamu ya kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
Huu Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 5, una mifano halisi na ya kutosha kumwezesha mwalimu kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu, utapata: 
• utangulizi wa kina kuhusu mtalaa wa umilisi 
• muhtasari wa umilisi, maadili, masuala ibuka na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa ufundishaji katika kila sura 
• matokeo maalumu, maandalizi ya somo na shughuli za ufunzaji wa kila somo mapendekezo ya majibu ya takribani maswali yote katika kitabu cha Mwanafunzi 
• mapendekezo ya shughuli za kutekelezwa na wanafunzi ili waendelee kujifunza wakiwa nje ya darasa 
• maswali ya ziada ili kukuwezesha kutathmini zaidi uelewa wa wanafunzi wako 
• maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi. 

Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwanafunzi na mwalimu wanahitaji ili kufaulu katika mtalaa huu wa umilisi.

ISBN: 9780195749069 SKU: BK00000001683
KES 450
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect