Phoenix Hatua za Kiswahili Rasmi GD4


Hatua za Kiswahili Rasmi, Kitabu cha mwanafunzi ni mfululizo wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa ufundi kwa kufuata 
mtalaa mpya unaosisitiza umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kukuza weledi wake katika stadi za kusikiliza na 
kuzungumza, sarufi na matumizi ya lugha, kusoma na kuandika. Vitabu hivi vina sifa zifuatazo: • Mada kuu zilizopangwa kwa 
kuzingatia ruwaza ya mtalaa ya Kiswahili Gredi ya 4 ili
kurahisisha utumiaji. Vipindi vilivyopangwa kushughulikia mada ndogo mbalimbali kulingana na ruwaza ya mtalaa.
Picha na michoro iliyochorwa kwa rangi za kupendeza ili kuvutia usomaji na ujifunzaji. • Maswali dodoso yanayochochea 
uwezo wa mwanafunzi kufikiria na kudadisi masuala
mbalimbali. Kazi za ziada na majaribio yanayomhusisha mwanafunzi binafsi, wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi kwenye 
makundi katika shughuli ainąaina. Mradi wa nyumbani unaowahusisha wazazi na walezi katika ujifunzaji wa Kiswahili na pia
kukuza uwajibikaji. · Hadithi na utajiri wa shughuli nyingine zinazokuza umilisi wa kimsingi wa lugha ya Kiswahili
na zilizooanishwa na masuala mtambuko, maadili chanya miongoni mwa masuala mengine.
Matumizi ya teknolojia kwa mfano kusikiliza sauti redioni na unasaji sauti kwa kutumia • simu na vifaa vingine vya 
kiteknolojia. Mathias Momanyi ni mtafiti, mwandishi, mwalimu na mwanahabari mashuhuri. Ameandika vitabu vingi vikiwemo 
msururu wa Kilele cha Insha vilivyosifiwa kwa ukwasi wake wa fani na tamathali za lugha komavu. Yahya Mutuku ni mwandishi 
na vilevile mwalimu mwenye uzoefu na utaalamu mkubwa. Ameshiriki kikamilifu katika harakati, na mikakati ya ukuzaji wa 
Kiswahili kupitia vipindi vya Kiswahili. Ameshirikiana na Mathias Momanyi kuandika msururu wa Kilele cha' Insha 
vilivyosifiwa kwa ukwasi wake wa fani na tamathali za lugha komavu. Pia ameandika hadithi nyingi pamoja na Kamusi ya Picha.
 

ISBN: 9799966479722 SKU: 2010127000835
KES 638
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect