Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu (Samakisa) Sekondari na Vyuo
by Y.M.Kihore, D.P.B.massamba, Y.P.Msanjila
Hiki ni kitabu kimojawapo katika mfululizo wa vitabu vya Sarufi vinavyotayarishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili katika jitihada zake za kukidhi mahitaji ya vitabu vya kufundishia somo la Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Kitabu kingine ambacho kilitayarishwa katika mfululizo huu ni idle cha Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA), ambacho kilichapishwa mwaka 1999. Vitabu hivi vimeandikwa kwa kuzingatia muhtasari wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo. Kitabu hiki kitawafaa wanafunzi na walimu wa sekondari, vyuo vya ualimu na hata vyuo vikuu. Wasomaji wa kawaida wa Kiswahili pia watanufaika nacho.

Reviews
This product does not have any reviews yet.
Add your review