Sauti ya Dhiki

by Abdilatif Addalla


Diwani hii - inayosheheni mashairi kuhusu utamaduni, mapenzi, nasaha, siasa, mambo ya kinyumbani, n.k. - ilitungwa baina ya 1969 na 1972 ambapo mtunzi alikuwa kifungoni baada ya kupatikana na hatia ya kuwachochea watu ili waipindue Serikali ya Kenya kwa kutumia silaha. Kwa hivyo, unapoisoma diwani hii hutaweza kujizuia kuona athari ambayo kifungo huweza kuwa nayo kwa mfungwa.Jambo la maana sana kuhusu diwani hii ni kwamba mtunzi ameweza kuzungumzia mambo ya kisasa, kama alivyofanya katika shairi la 'Usiniuwe!', bila kupotoka na kutafuta mifano ya kigeni. Hili ndilo lililompa Shihabuddin Chiraghdin, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, kusema katika utangulizi wake kwamba, ingawa mtunzi ameingiliwa na athari za kigeni kwa ajili ya elimu aliyoipata shuleni, 'hakukubali kuzongwazongwa na athari hizo, hivyo mashairi yake hayana maingilio ya miundo ya kigeni hata chembe, na mawazo yake yote yameambatana na Uswahili na Uafrika kwa jumla'.Kitabu hiki kitawafaa wale wapendao kusoma mashairi ya Kiswahili ya kiwango cha juu, na vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vikuu.

ISBN: 9780195738193 SKU: 2010143000355
KES 510
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect