Storymoja: Shajara yangu ya klabu ya usomaji Kiwango 2

by Story Moja

by Storymoja


Ikiwa unataka kuwa mwerevu zaidi, mjuzi na mwenye kuvutia, soma vitabu vingi zaidi vya hadithi. Ikiwa unapania kuwa mbunifu zaidi ili siku moja uweze kuwa mvumbuzi au mjasiriamali, soma vitabu vingi Zaidi vya hadithi. Ikiwa unataka kazi yenye mapato mazuri na kuchangia katika maendeleo ya taifa katika siku za usoni, soma vitabu vingi zaidi vya hadithi.

Jaza shajara yako kila wakati unaposoma. Onyesha wazazi au mlezi shajara yako na uwaambie kuhusu vitabu ambavyo umevisoma. llinganishe shajara yako na za marafiki zako kisha msherehekee usomaji wenu iwapo mmesoma vitabu vingi. Kusoma kunawezesha! Kusoma ni poa. Kusoma kuna manufaa kwako!

MZAZI: SOMA PAMOJA NA MTOTO WAKO

Furahia uhondo wa kusoma pamoja na mtoto wako. Mtoto wako atavipenda vitabu maishani mwake na atajifundisha kwa wepesi endapo utazingatia hoja kumi rahisi zilizoorodheshwa hapa chini.

1. Soma pamoja na mtoto wako katika mazingira yaliyotulia kama vile kwenye chumba cha kulala.

2. Mhimize mtoto wako awe na mazoea ya kusoma hadithi nzima kwa kutumia viziada vya lugha kama vile kupandisha sauti.Asome hadithi nzima kwanza akilenga kuifurahia tu kisha aisome tena ili ajue yaliyomo. |

3. Mhimize mtoto wako ayaashirie maneno kwa vidole hasa anaposoma hadithi aliyokwisha kuisoma awali.

4. Chunguza kama mtoto wako anaelewa aliyoyasoma kwa kumuuliza maswali kuhusu michoro, wahusika na hadithi mara kadhaa.

5. Kuwa na mtazamo chanya kuhusu hatua anayopiga mtoto wako katika usomaji wake. Usimvunje moyo bali umsifu kwa kila hatua anayopiga.

6. Hakikisha kwamba mtoto wako anaisoma hadithi mara kadhaa.

7. Baada ya mtoto wako kuzoea kusoma hadithi fulani, mhimize ajaribu kukusomea baadhi ya maneno ya hadithi hiyo au hadithi nzima.

8. Mnunulie mtoto wako vitabu tofauti tofauti vya kuburudisha kama vile vitabu vya picha, vya kuchekesha na vya kuelimisha.

9. Mwonyeshe mtoto wako kwamba una nia ya kufuatilia na kujua hadithi anazozisoma kwa kumuuliza maswali kuhusu hadithi hizo. Pia mhadithie hadithi ulizosoma kwenye vitabu ulivyo navyo.

10. Uwe kielelezo bora kwa mtoto wako ili avithamani vitabu. Mwache mtoto wako akuone wewe ukisoma vitabu vingi.

ISBN: 9789966621948 SKU: 2010127000798
KES 480
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect