Shamba la Halaiki

by Spotlight Publishers


Shamba la Halaiki ni tamthilia inayomulika hall halisi ya uongozi katika jamii inayowashangilia na kuwakashifu viongozi kwa msingi wa kikabila. Wakazi wa Mabondeni katika Jimbo la Matengo wanakumbwa na mafuriko yenye maangamizi makubwa. Halaiki, mmiliki wa shamba kubwa lenye rasilimali nyingi, anatoweka punde to mafuriko yanapotokea. Kutoweka kwake kunazua maswali na taharuki. Je, alisombwa na maji? Je, alivawa?Je, angali hai? Vuta n'kuvute baina ya Gavana Mbi na wafuasi wake kwa upande mmoja na Seneta Lila na wandani wake kwa upande wa pili kuhusu fedha za kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko na umiliki wa shamba la Halaiki inachora taswira halisi ya jamii inayowashangilia waovu na kuwasulubu wema. Je, hatima yake ni nini? Je, pana chembechembe ya matumaini katika jamii kama hii? 

ISBN: 9789966570314 SKU: 2010129000185
KES 522
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect