Siri Sirini 2: Mpiga Mbizi Kilindini kitabu cha 2

by Rocha M.Chimerah


Ni nani aliyetenda kitendo hiki kilichobakia kuwa siri ya kughasi, siri iliyo sirini? Ni Kidhabi au ni Kijumwa? Hiki ni kitendo kipi ambacho kimebaki kuwa siri iliyofichika, isiyojulikana na wazee wa mji wala vijana wa kijiji, viongozi au waongozwa? Ni kitendo gani hiki ambacho kinaumiza vichwa vya wafalme na vitwana, maimamu na maimuma, hadi mfalme anapatwa na kizunguzungu kwa kupiga mbizi kilindini? Na si yeye tu, bali lukuki ya watu! Kero inapozidi kero na siri inapozidi kusaki sirini, mfalme anariaria na kuendelea kupiga mbizi... 'Mfalme alishtuka. Mfalme alihangaika, mfalme alibabaika. Alipiga mbizi katika marefu na mapana ya akili yake... Ni nani aliyefanya kitendo hiki? Kwa ajili gani? Alikifanya yeye peke yake au kwa ushirika na wengine?

ISBN: 9789966368195 SKU: 2010129000167
KES 755
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect