Stadi za Kiswahili Shugli za Lugha Kitabu cha Mwanafunzi Gredi 2

by Mwalimu Kipande

 • ISBN: 9789966630308
 • SKU: 2010127000700

Stadi za Kiswahlli ni Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2 ni kitabu cha ziada kilichoandakwa kwa mujibu wa mtaala mpya uegemeao umilisi uliozinduliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD) mnamo Septemba 2017. Kitabu hiki kimejumuisha mada zote kuu na ndogo zilizomo katika ruwaza ya mtalaa ya Kiswahili Gredi ya 2. Isitoshe, mada kuu na ndogo zimepangwa kulingana na jinsi zilivyopongwa katika ruwaza hiyo. Fauka ya haya, yaliyomo yamewasitishwa kwa ubunifu wa hali ya juu kuyaoanisha na umilisi wa kimsingi, masuala mtambuko, maadili miongoni mwa masuala mengine yanayofumbatwa na mtaala mpya uegemeao umilisi. Kitabu hiki kimejumuisha shughuli za aina nyingi za kufanywa na mwanafunzi binafsi, wanafunzi wawili wawili na makundi ya wanafunzi. Kazi na shughuli za wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi katika makundi zinadhamiriwa kuimarisha stadi za kusikitiza na kuzungumza na vilevile umilisi wa ushirikiano na mawasiliano. Aidha, kitabu hiki kimesheheni vifungu vya kusoma na vya kuchangamsha vitakavyomsaidia mwanafunzi kuimarisha stadi ya kusoma. Stadi ya kuandika haijaachwa nyuma. Kitabu kinazo shughuli za kutosha za mwanafunzi iii kustawisha stadi ya kuandika. 

KES 285

Customer Reviews

This product does not have any reviews yet - be the first to write one.

You may also like

 1. Jifunze Kiswahili Darasa la 2
  Jifunze Kiswahili Darasa la 2
  by Lucy W.Muriithi
  KES 290
 2. Mwanasayansi 2f
  Mwanasayansi 2f
  by Egara Kabaji
  KES 195