Tamthilia ya Maisha

by Wamitila


Tamthilia ya Maisha ni mkusanyiko wa mashairi bulibuli na diwani ya kwanza ya aina yake kuwahi kuchapishwa. Diwani hii inaleta pamoja tungo za arudhi na tungo huru zilizotungwa na washairi tofauti wa Afrika Mashariki. Dhamira za mashairi yaliyomo zinatanda mwanda mzima wa maisha: kero na migogoro yetu, mahusiano yetu, siasa na tamaa zetu, ndoto na hofu zetu pamoja na unafiki, uoza na uthori uliotamalaki jamii zetu. Dhamira hizi zimewasilishwa kwa mitindo aali na yenye ubunifu usiomithilika. Hii ni diwani itakayopekecha hisia na kumtia msomaji upupu wa kutamani kuibadilisha jamii yake. Ni tamthilia inayomwalika msomaji auone uigizaji wake na wa waja wenzake kwenye jukwaa hili la maisha. Hii ni dafina itakayomweka kama Zuhura kwenye anga ya Fasihi ya Kiswahili kwa miaka mingi ijayo.

ISBN: 2010129000039 SKU: 2010129000039
KES 475

You can get an email alert when this product is back in stock.

International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect