Tesi na mwalimu paka

by Story Moja

by Nyaga


Mwalinu paka ana wanafunzi wenye bidii masomoni. Tesi ni mmoja wa wanafunzi hao. Anawatuza wanafunzi wake kwa bidii zao. Katika harakati ya kuwatuza, pesa zake zinapotea. Je, ni Tesi ama ni nani aliyezichukua pesa hizo? Je, pesa hizo zitapatikana?
Mtoto wako ni wa kiwango gani cha usomaji? Tumia vigezo vifuatavyo kubainisha kiwango cha mtoto
 wako ili umpe vitabu mwafaka kulingana na uwezo wake wa kusoma. Hivi ndivyo vidokezi: KIWANGO CHA MWIBUKO (A, B, C).
Msomaji anajifundisha kuhusisha neno na picha. Msomaji anajifundisha kutambua herufi na nambari.
 Msomaji anaweza kutambua picha zenye uhalisia pekee.
KIWANGO CHA MWANZO (D, E, F)
Msomaji anakuza uwezo wake wa kutambua maneno. 
Msomaji anakumbuka maneno kwa urahisi anapoyarudia. 
Msomaji anafahamu hadithi kwa kutegemea picha.
MA
KIWANGO CHA MPITO (G, H)
Msomaji anajifundisha kusoma kwa ufasaha na kuigiza vitendo na hisia. 
Msomaji hategemei sana picha kuelewa hadithi. 
Msomaji anatambua na kufurahia mitindo tofauti ya picha.
KIWANGO CHA KATI (1,1)
Msomaji anasoma bila kutegemea kusaidiwa. 
Msomaji anafurahia kusoma hadithi za aina tofauti.. 
Msomaji anaweza kusoma na kuelewa hadithi zenye ujumbe tata.
 

ISBN: 9789966621054 SKU: 2010143001032
KES 420
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect