Test it and Fix it KCSE Kiswahili: Ijaribu na Uikarabati

by Ipara


Ukarabati wa matokeo bora ya KCSE ndio huu! Test it & Fix it: KCSE Revision ni nembo ya mfululizo mpya wa vitabu unaokidhi kwa kina mahitaji ya silabasi ya sekondari. Kila kitabu kina mazoezi yaliyotayarishwa na mabingwa katika nyanja zao ili kuwasaidia watahiniwa kutambua shida zozote walizonazo kwenye somo mahususi na kuzitatua. Kwa nini Ijaribu na Uikarabati? Ijaribu na Uikarabati: Marudio ya KCSE Kiswahili kinakupa:

  •  Vidokezo vya mambo ya kuzingatiwa katika mtihani. 
  •  Mifano kabambe ya maswali ya mtihani kwenye ufahamu na ufupisho, isimujamii, fasihi simulizi na fasihi ya vitabu teule.
  •  Mazoezi chungu nzima ya sarufi ya kujipima na kuimarika. 
  •  Mifano chekwachekwa ya tungo zitakazowaongoza watahiniwa kuandika aina mbalimbali za insha. 
  • Zoezi la ziada mwishoni mwa kila sura ili kuimarisha uelewa. 
  •  Michoro ya kurahisisha uelewaji wa somo. 
  • Mitihani miigo ya kuwaandaa watahiniwa kukabiliana na maswali ya mtihani wa KCSE.
  • Majibu ya maswali yote mwishoni mwa kitabu.
ISBN: 9780195737646 SKU: 2010127000230
KES 800
International delivery
Free delivery on orders over KSh 2,000
Free click & collect