Tumaini la Nimara (Story Moja)

by Story Moja


MSURURU WA STADI ZA MAISHA WA STORYMOJA Yusufu Miremba ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi na miwili nchini Uganda. Mpango wa wanafunzi kuandikiana barua unaanzishwa baina ya shule yao na nyingine nchini Sri Lanka. Kupitia kwa mpango huo, Yusufu anapiga urafiki na Nimara de Silva kwa njia ya kuandikiana barua Genge la wanamgambo linamteka nyara Yusufu na kutokomea naye mwituni. Nimara anaanzisha kampeni ya kumwandikia barua kiongozi wa genge hilo pamoja na wengine wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni akiomba Yusufu aachiliwe huru. Haya yote yakiendelea, Yusufu anakula mwata mwituni. Je, kampeni za Nimara zitafua dafu? Je, Yusufu ataachiliwa huru? Watawahi kuonana ana kwa ana?

SKU: 2010143000892
KES 450
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect