Zinguo la Mzuka

  • ISBN: 2010129000192
  • SKU: 2010129000192

Ujasiri, ari na azma inayozua michomo mikali ya kujipata upya pamoja na kurejesha urazini; inafanya watu waliozoea 
kukimya na kutazama madhabahu yao yakinajisiwa kufurukuta. Hii ni tamthilia inayoangazia maswala nyeti kama: ujenzi wa 
jamii mpya, uongozi, ukiritimba, ubinafsi na uozo mwingine wa kijamii. Isitoshe, inamulika uhusiano wa nchi huru za 
Kiafrika na nchi za Magharibi.
Leo Sanja Leonard anatia guu tena katika uga wa fasihi na hii tamthilia inayozua hisia nzito. Mbali na kuwa mshairi, 
baadhi ya kazi zake ambazo zimechapishwa ni pamoja na; Mimba Ingali Mimba katika diwani ya Mimba Ingali Mimba na Hadithi 
Nyingine, Kasalia katika Shingo ya Mbunge na · Hadithi Nyingine na Kurunzi ya Kiswahili.
 

KES 348

Customer Reviews

This product does not have any reviews yet - be the first to write one.