JKF Nyota ya Kiswahili GD1 Trs (Approved)


Huu ni mwongozo unaompa mwalimu mbinu za kumwezesha kuchochea ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi kuambatana na mtalaa mpya. Mtalaa huo unampa mwanafunzi uwezo wa kujifunza mwenyewe huku mwalimu akiwa msaidizi woke.

Kitabu hiki kinampa mwalimu mapendekezo ya hatua anazoweza kufuata ili kumwongoza mwanafunzi aweze kujifunza kila mada ndogo kuambatana na maarubu ya mtalaa wa kiwango husika.

Ili kumwezesha mwalimu ayatimize malengo yake, mwongozo huu umemwandalia ratiba ya mafunzo ya mwaka mzima kwa mtiririko ufuatao:

° Matokeo maalumu yanayotarajiwa mwanafunzij kuweza kuyafanya kufikia mwisho wa mada husika

° Umilisi wa kimsingi

° Maadili ya kimsingi

° Masuala mtambuko

° Uhusiano na masomo mengine

° Uhusiano na shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji

° Uhusiano na shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji

° Nyenzo

° Tathmini

Kitabu hiki pia kinatoa mazoezi ya ziada ambayo wanafunzi watapewa na mwalimu ili wajifunze zaidi.

Waandishi walioandika mwongozo huu ni wenye tajiriba kubwa. Wamehusika na uandishi wa vitabu vya kiada kwa muda mrefu. Vitabu vyao vinaendelea kutumika hadi leo.

KES 513
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect