Kifunganjia

by Daniel Okello


Kifunganjia ni tamthilia inayotoa taswira halisi ya masuala mbalimbali yanayozuia au kudidimiza harakati za maendeleo na ufanisi katika nchi zinazoendelea kukua kiuchumi.

Kijiji cha Bakunja kinategemea kilimo. Wakulima wanatarajiwa kuhifadhi sehemu ya nafaka katika ghala la kijiji kwa ajili ya matumizi ya baadaye hasa msimu wa ukame. Hata hivyo, nafaka wanazoweka ghalani hutoweka. Ghala halijai. Rajua, kijana ambaye anaongozwa na msukumo wa kuleta mabadiliko mazuri katika jamii kupitia uanahabari na uigizaji, anaamua kubomoa ua unaolizingira ghala ili wanakijiji wajionee kinachojiri ghalani. Wizi uliokithiri ghalani na uwepo wa panya na mchwa unadhihirika. Huku hays yakijiri, wasimamizi wa ghala na wapinzani wao wanakula na kustarehe. Hali hii inafanya Baraza la Wazee kuchukua hatua ya kuwatuma vijana wa kijijini maabarani ili washiriki katika utafiti wa kuvumbua dawa za kuulia panya na mchwa waharibifu. Rajua kwa upande wake anaendeleza juhudi za kuleta mabadiliko katika usimamizi wa ghala. Anawania wadhifa wa kulisimamia ghala ill wanakijiji wapate haki. Je, juhudi za Rajua zitaz.aa matunda? Atafaulu kuchaguliwa kuwa msimamizi mpya wa ghala? Vijana waliotumwa kufanya utafiti maabarani watawafaa wanakijiji? 

ISBN: 9789966623768 SKU: BK00000005182
KES 350 KES 450
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 3,000
Free click & collect

Reviews

This product does not have any reviews yet.

Add your review