Wema Hauozi (Access)
Wema Hauozi ni tamthilia fupi inayochunguza mgonganokati ya wenye tamaa ya kutenda maovu na wenye kero dhidi ya tamaa hiyo. Mgongano huu una madhara makubwa kwa wenye ujasiri wa kukemea maovu hayo lakini yote hayo ni kwa muda tu. Kumbe ipo siku juhudi za kuuzika wema hushindwa na badala yake mbegu ya wema huchipuza na kuzagaza matawi yake kwa kila kiumbe kuona. Tamthilia hii yenye ucheshi imeandikwa kwa ufundi mkubwa unaokuacha ukiwa unajiuliza maswali ya kufikirisha ufikapo mwishoni.
Dkt. Timothy M. Arege ni mwandishi wa tamthilia, mashairi na hadithi fupi. Tamthilia zake nyingine ni Chamchela, Mstahiki Meya, Kijiba cha Moyo, Majira ya Utasa, Duara, Si Shwari na Bembea ya Maisha. Kwa sasa Arege ni Mhadhiri Mkuu katika Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Kenyatta.