Kamusi Angaza kwa Shule za Msingi

by Ahmed E.Ndalu


Kamusi Angaza kwa Shule za Msingi ni zao la utafiti wa kina uliofanywa na mwandishi na wanaleksikografia. Kamusi hii imetungwa kwa utaalamu mkuu na kwa kuzingatia msomaji lengwa. Miongoni mwa sifa za kamusi hii zinazodhihirisha upekee wake ni:

  • zaidi ya vidahizo 7,000
  • takriban maneno 170,000
  • ngeli zimebainishwa ifaavyo
  • mifano ya sentensi kwa Kiswahili sanifu
  • picha za kuvutia msomaji
  • kiambatisho kinachojumuisha picha za wanyama, maumbo, rangi na aina nyingi za ndege.

Kwa msingi wa sifa za kamusi hii, ni dhahiri kuwa kwa kuitumia, mwalimu na mwanafunzi watakuza msamiati, kufahamu ngeli na matumizi yake na vilevile matumizi ya kidahizo husika kutunga sentensi sahihi kisarufi.

ISBN: 9789966258083 SKU: 2010127000521
KES 653
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect