Kamusi Fafanuzi ya Methali

by Timothy Arege, Mwalaa Nyanje


Kamusi Fafanuzi ya Methali ni kitabu muhimu sana kwa wanafunzi na walimu wa shule za msingi na upili. Kitawafaa wanafunzi wa vyuo vya ualimu na vyuo vikuu pamoja na watafiti na wapenzi wa lugha ya Kiswahili katika viwango vyote.

  • Jumla ya sifa za kamusi hii ni:
  • Mkusanyiko wa methali 3,536.
  • Methali zimepangwa kwa utaratibu wa kialfabeti ili kuwezesha urejeleaji rahisi.
  • Msamiati mzito umeelezewa ili kumwepushia msomaji utata wa maana.
  • Maana ya juu/kawaida na maana batini/ya ndani za kila methali zimefafanuliwa kwa lugha rahisi inayoeleweka na wasomaji wa viwango vyote.
  • Matumizi zaidi ya moja yametolewa katika methali nyingi.
  • Methali zilizo sawa au kinyume kimaana na kimatumizi zimeelekezwa.
ISBN: 9966002413 SKU: 2010127000478
KES 945
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect