Mji wa Matarajio (One Planet)


Daktari Jemima aliisoma barua hiyo. Muda wote huo, Herina alikuwa anamtazama tu. Aliona macho ya Jemima yakitua kwenye neno fulani na kumtazama, ila hakujishughulisha kuhusu mtazamo huo. Alimaliza kusoma barua hiyo na kushusha pumzi. Alimtazama Herina, kisha Jeff na hatimaye ile barua. Herina aliona vipira vya machozi vikijitokeza machoni mwa mwajiri wake. Hata hivyo, kwenye vipira hivyo aliona mwanga wa matumaini...

Ulanguzi wa binadamu unamnyima Herina nafasi ya kujiendeleza kielimu wakati ufaao. Hata hivyo, Herina anaichukua changamoto hii kama njia ya kuifunza jamii yake kuhusu thamani ya binadamu, hata wale wenye mahitaji maalumu. Herina ni kielelezo cha vijana wanaojiamini na ambao hawakati tamaa hata wanapokabiliwa na changamoto
kali. Tembea naye katika hadithi ya Mji wa Matarajio ili ujifunze mengi.

KES 300
International delivery
Free delivery on orders over Ksh 2,000
Free click & collect
UPCBK00000008752
Author Assumpa K.Matei
ISBN 9789914410068
SKUBK00000008752

Reviews

Leave a product review
or cancel